Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne 2018 na Matokeo ya QT

logo ya mwalimu makoba

Matokeo ya Kidato cha Nne

Matokeo ya kidato cha nne, yametangazwa na baraza la mitihani. Bofya link hapo juu kuona matokeo yote.

Matokeo ya Mtihani wa Upimaji Maarifa QT


Endapo link hiyo inasumbua, jaribu hii chini...

Asemavyo Mwalimu Makoba Kuhusu Matokeo ya Kidato cha Nne na QT Mwaka 2018

Kila yanapotoka matokeo ya kidato cha nne, hunikumbusha wakati nami nilipokuwa nikiyasubiri matokeo yangu enzi zile ndiyo nimehitimu kidato cha nne. Natambua ugumu wa kuyatazama matokeo hasa yanapokuwa mabaya. Hata yanapokuwa mazuri, bado kuna hofu, maana safari ya masomo bado kukoma.Huenda ukasoma kidato cha tano, huko utafanya tena mtihani wa kidato cha sita. Ukifika chuo nako, utakutana na mitihani ya kila mara ambayo ukiishindwa, hutaweza kuendelea na masomo bila kujali kuwa ulifaulu kidato cha nne, ulifaulu kidato cha sita. Hivyo, bado safari ni ndefu na haitakiwi kubweteka, juhudi ndiyo msingi pekee wa mafanikio.

Nawapongeza wanafunzi wote, waliofanya vizuri na waliofanya vibaya. Waliofanya vizuri, wazidi kusonga mbele, elimu ya kidato cha nne, ni mwanzo tu, bado vidato vingi vinakuja huko mbele. Bidii na kujituma, kunapaswa kuongezeka zaidi. Kama umeweza leo, amini unaweza hata kesho.

Ushauri Kwa wanafunzi waliofanya vibaya

Siyo mwisho. Usikate tamaa. Bado unanafasi ya kujaribu tena. Watu wengi waliofanikiwa, waliwahi kushindwa pia. Matokeo haya, yawe somo kwako, tambua ni kipi kimekufanya ushindwe, kisha sema, "sitashindwa tena, mimi ni mshindi!"

Wewe si wa kwanza kushindwa, wapo wengi walioshindwa, wakasikitika, lakini wakasimama tena na kujikuta wakifanikiwa. Amini ya kwamba wewe ni mshindi na unaweza kupambana tena na tena.

Kubali kuwa umeshindwa, kisha tafuta namna bora ya kushinda. Hatua ya kwanza ya kuondoa tatizo, ni kulikubali kwanza. Huna sababu ya kupoteza furaha kwa sababu ya matokeo ilhali unanafasi nyingi tu za kupambana na kuweza kuyabadilisha matokeo hayo hata kama ni mabaya sana.

Bado unanafasi nyingine. Unaweza ukarudia tena. Endapo utahitaji kurudia tena masomo yako, hakikisha unasoma katika sehemu inayostahili. Usisome katika eneo ambalo litakuwa sababu ya wewe kushidwa na kukata tamaa. Bado wewe ni mshindi, huu ni mwanzo tu!

Kwa masomo wasiliana na Mwalimu Makoba kwa namba:

0754 89 53 21 au 0653 25 05 66

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu