Mtihani wa Kiswahili 2 Kidato cha Sita| April 2018

Mtihani wa Kiswahili 2 Kidato cha Sita| April 2018

JINSI YA KUUFANYA MTIHANI HUU

Mtu yeyote na kokote aliko anaruhusiwa kufanya mtihani huu.

Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi.

Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba, 0754 89 53 21.

Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho.

Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000 (elfu mbili) tu.

Namba za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 na Tigo pesa 0653 25 05 66

“Kwa kuwa lengo la mtihani huu ni kutaka kujua uwezo na mapungufu ya mwanafunzi ili aweze kupewa mbinu mbadala za kumsaidia kufaulu mtihani wake wa mwisho, kuangalizia majibu hakuna faida yoyote kwani lengo la mtihani si kubaini nani atakuwa wa kwanza na yupi atakuwa wa mwisho!”

Mwalimu Makoba| Mwalimu wa Waalimu na Wanafunzi| Mwalimu wa Ushindi!

Unataka kufanya mtihani huu na hujaelewa taratibu zake? Wasiliana na Mwalimu Makoba kwa 0754 89 53 21.

Sasa fanya mtihani wako.

Tumia masaa matatu kuufanya mtihani huu

Sehemu A (alama 20)Fasihi kwa Ujumla

1. Jadili mabadiliko ya tamthiliya katika vipindi mbalimbali. Toa hoja tano.

Sehemu B (alama 20)Ushairi

2. “Mshairi mzuri ni yule anayeionya jamii yake.” Jadili ukweli wa kauli hiyo kwa kutumia diwani mbili ulizosoma. Hoja nne kwa kila kitabu.

Sehemu C (alama 20)Riwaya

3. Mwanamke huchorwa katika pande mbili, mwema na mbaya.” fafanua kauli hii kwa kutumia hoja nne kwa kila riwaya.

Sehemu D (alama 20)Tamthiliya

4. Jadili matatizo manne kwa kila tamthiliya ambayo mwandishi hakuyatolea masuluhisho.

Sehemu E (alama 20)Usanifu wa maandishi

5. Soma habari ifuatayo kisha jadili mbinu za kifani zilizotumika.
Katika chumba changu cha upweke, chumba cha kuchakata fikra na kufanya maamuzi sahihi mabadiliko kiasi yametokea. Hayajatokea ndani, la hasha! Purukushani hizi ziko nje, nje ya chumba, chumba cha upweke!
Mwanzo nilikuwa nikisikia watu wakinong’ona kwa sauti za chini kama sisimizi. Sikuweza kumaizi ni kipi hasa walichokuwa wanajadili, sikujali nilijua ni minong’ono ya watembea bure ambao ama hakika si sawa na wakaa bure.
Muda ulivyozidi kwenda, minong’ono ikakua na kuwa sauti kubwa iliyosikika dhahiri masikioni mwangu.
“Umetusaliti… umetusaliti… umetusaliti…”
Sauti hizi nazisikia kila siku sasa, hata hivyo maneno mengine yameongezeka na kutengeneza mseto safi wa hoja.
“Mwalimu wa waalimu umenunuliwa… husemi tena, wamekufunga mdomo… umetusaliti, umetusaliti, umetusaliti. Lakini hutabaki salama, u wapi u gwiji wako na mbwembwe za kukata njuga za wala vinono?”
“Hakuna awezaye kuninunua, nitakata gidamu za mjinga yeyote!” najibu kwa kujiamini, sauti inatoa kicheko cha matumaini, kisha ina bwabwaja,
“Kama ni hivyo, basi yaseme yanayotusibu, ukikaa kimya kidagaa kitatuozea mwalimu…”
“Mimi ndiye kombora la kudungua makombora, kama kuna mchafu koge nitasema,” najibu kwa kujiamini.
Sauti za watu ni sauti ya Mungu. NITASEMA NA HAKUNA WA KUNINYAMAZISHA!

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie