MAREKANI YAKUMBWA NA BALAA JINGINE

marekani kimbunga irma

Misukosuko imezidi kuiandama nchi ya Marekani. Baada ya kuibuka kwa matukio mengi ndani ya kipindi cha muda mfupi ikiwemo mashambulizi ya kigaidi, hatimaye janga jipya limechomoza.
Kimbunga kinachotambulika kwa jina la Irma kinatajwa kupiga kisiwa cha Marco huko Pwani ya Florida.


Upepo wake ni hatari na unakadiliwa kuwa na kasi ya Kilomita 192 kwa saa. Hata hivyo, kimeelezwa kushuka na huenda hali ikawa shwari.
Hasara ya kuanguka na kuharibika kwa majengo zaidi ya milioni 3.4 na kukosekana kwa umeme ni miongoni mwa maafa yaliyolikumba jiji la Florida.

Vifo vitatu vimetajwa kusababishwa na kimbunga hicho. Pia huenda kikaendelea kufanya uharibifu mkubwa zaidi.

TAZAMA POVU LA MWALIMU MAKOBA KWA WASANII WAVAA HOVYO...

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Vichekesho vya Kuchekesha na Kuvunja Mbavu 1