MAJARIBIO YA KOMBORA LA KOREA YASABABISHA MADHARA

MAJARIBIO YA KOMBORA LA KOREA

Picha za Satelite zilizopigwa, zimetoa majibu juu ya madhara yaliyosababishwa na majaribio hayo. Korea kasazini ambayo ni kinara wa majaribio ya makombora ya Nyuklia, imesababisha mmomonyoko mkubwa wa ardhi ukiambatana na utelezi.
Korea ya Kaskazini imefanya majaribio sita ya nyuklia. Taarifa zimethibitisha kuwa, picha za hivi karibuni zinaonyesha mmomonyoko mkubwa wa udongo na utelezi katika maeneo yalikotumwa makombora.
Uharibifu huo umetokea katika eneo la mlima Mantap. Pia wataalamu wameeleza hali hiyo inaweza kusababisha mlipuko wa volcano.
Korea Kaskazini imekuwa ikiendesha majaribio mengi ya Nyuklia suala ambalo haliungwi mkono na mataifa mengi ikiwemo Marekani.


IMEANDIKWA NA: MOWASHA| NGEME

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne