Kiswahili pre NECTA 5
Sehemu A
1. Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali.
Ilikuwa usiku wa manane niliposikia kelele za watu nje
ya nyumba yetu ya nyasi. Niliamka haraka kisha nami nikaelekea nje ili nikapate
kujua kilichokuwa kikiendelea. Huko nje nilikuta watu wote wamesimama wakipiga
kelele huku wakiwa wameangalia juu.
“Mwizi! Mwizi! Mwizi!”
Nami nilitazama juu ili nione kilichowaliza, Loooh!
Nilikiona kijitu kichafu kimevaa koti jeusi toka sayari ya mbali kikiwa
kimeubeba mwezi wetu kikikimbia nao kuelekea mbali huko juu angani. Kabla
sijashusha uso wangu chini giza kuu liliingia hata hatukuweza kuonana.
Vijana wa usalama wa nchi, waliwasha mienge ya moto
hapo tuliweza kuonana tena, wote tulikuwa na masikitiko makubwa. Nilimuona mama
na kaka yangu Mowasha wakilia kwa huzuni.
Maswali
a. Kipi
kiliibwa hata watu wakapiga kelele za kuita mwizi
b. Kwa
nini Mowasha alilia kwa huzuni?
c. Unadhani
tukio linalozungumziwa kitabuni linaweza kutokea katika maisha halisi? Kwa
nini?
2. Fupisha
habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua 30 na yasiyozidi 40.
Sehemu B
3. Toa tofauti mbili zilizopo kati ya sentense na kishazi
4. Orodhesha
mambo manne ambayo ndiyo sababu ya utata katika lugha
Sehemu C
5. Wewe ni mwanafunzi ambaye unatarajia kuhitimu kidato cha nne, andika risala itakayosomwa mbele ya mgeni rasmi siku ya sherehe.
Sehemu D
6. Upi ulikuwa mchango wa waingereza katika kuikuza lugha ya kiswahili? Toa hoja nne zilizopambwa kwa mifano.
Sehemu E
Chagua maswali matatu
katika sehemu hii. Swali la 10 ni la lazima
7. Jadili mafunzo mbalimbali yanayopatikana katika diwani mbili ulizosoma
8. Waandishi
ni watu ambao hutumia muda wao mwingi kuwatetea wanyonge. Thibitisha ukweli wa
kauli hii kwa kutumia tamthiliya mbili
9. Chagua mhusika mmoja katika kila tamthiliya uliyosoma, kisha jadili sifa zake
10. Tunga ngano kuhusu kisa chochote cha kusisimua